Majmaa-Ilmi inahuisha siku za Lailatul-Qadri katika mji wa Baabil na Hindiyya.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu imehuisha siku za Lailatul-Qadri katika mkoa wa Baabil na wiliya ya Hindiyya.

Ibada za Lailatul-Qadri zimesimamiwa na tawi la Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa katika mkoa wa Baabil na wilaya ya Hindiyya.

Tawi la Maahadi katika mji wa Baabil limefanya ibada za Lailatul-Qadri kupitia ratiba ya Multaqa-Nurain awamu ya pili, iliyofanywa kwa kushirikiana na uongozi wa mazaru ya Alawiyya-Sharifa, kundi la wasomaji wa Qur’ani limeshiriki kwenye ratiba hiyo pamoja na mazuwaru wa malalo takatifu.

Tawi la Maahadi katika wilaya ya Hindiyya limefanya makumi ya vikao vya usomaji wa Qur’ani na dua maalum za Lailatul-Qadri.

Ratiba ya Lailatul-Qadri inalenga kuhamasisha utendaji wa ibada za usiku na kuhimiza waumini kunufaika na siku hizi tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: