Kitengo cha Dini kimehitimisha majlisi za kuomboleza katika mji wa Mosul.

Majlisi zimesimamiwa na kituo cha utamaduni na maendeleo chini ya kitengo cha Dini.

Mkuu wa kituo Shekhe Haidari Aaridhi amesema “Majlisi ni sehemu ya harakati za Atabatu Abbasiyya ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika wilaya ya Sanjaar, zimehudhuriwa na kundi kubwa la wakazi waliokuja kuomboleza kifo cha Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) pamoja na kufanya ibada za Lailatul-Qadri”.

Akaongeza kuwa: “Kituo kiliandaa ratiba maalum iliyodumu kwa muda wa siku tatu, kuanzia usiku wa mwezi kumi na tisa Ramadhani, ambapo zimetajwa sifa za kiongozi wa waumini (a.s) na umuhimu wa kufuata mwenendo wake”.

Ratiba ya ibada ilipambwa na usomaji wa qaswida na mashairi ya kumsifu Imamu-Mutaqina (a.s), zikafuata ibada za usiku wa Lailatul-Qadri zilizo funguliwa kwa kusoma Qur’ani tukufu na dua ya kunyanyua misahafu pamoja na swala za suna zilizopokewa katika siku hizo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: