Katika jengo la Kuleini.. Atabatu Abbasiyya inatoa futari kwa mazuwaru wa Ataba mbili tukufu.

Atabatu Abbasiyya inatoa futari kwa mazuwaru wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika jengo la Shkhe Kuleini.

Makamo rais wa jengo hilo Mhandisi Ahmadi Haamid Sarhani amesema “Tunapokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) siku zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa “Kila siku tunagawa futari kwa mamia ya mazuwaru, wanaokuja kutokea upande wa mji mkuu wa Bagdad, kwani jengo lipo upande wa barabara ya Bagdad-Karbala, akasema kuwa ratiba hii inaendelea hadi mwisho wa mwezi wa Ramadhani”.

Akabainisha kuwa “Ataba tukufu katika kila msimu wa mwezi wa Ramadhani hugawa futari kwa mazuwaru kupitia majengo tofauti yaliyo chini yake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: