Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasi kimetoa chapisho jipya la kitabu cha Wahyi na Utume katika Qur’ani.
Kitabu hicho kimeandaliwa na kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni.
Nacho ni sehemu ya mfululizo wa vitabu vya masomo ya Aqida vilivyo andikwa na Shekhe Abdullahi Jawadi Aamiliy na Sayyid Hashim Milani.
Muandishi amelenga kuthibitisha asili ya Utume kwa kutumia mfumo wa ulimwengu, aya za Qur’ani tukufu, riwaya tukufu na dalili za kiakili.