Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s).

Chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s) kwa wanafunzi wa bweni na kuandaa futari ya pamoja.

Majlisi hiyo imefanywa kwenye bustani za chuo kwa ushiriki wa wanafunzi wa bweni.

Shughuli hiyo imefanywa chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, chini ya usimamizi wa rais wa chuo Dokta Muayyad Imran Alghazali.

Baada ya majlisi wakala futari ya pamoja katika eneo la bustani na uwanja wa michezo, mada kuu ilikuwa ni wajibu wa mzazi kwa mwanafunzi wa chuo, sambamba na utukufu wa siku za Lailatul-Qadri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: