Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya anajadili njia za kushirikiana na muwakilishi wa Waziri wa mipango.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, amejadili njia za kushirikiana na ujumbe kutoka wizara ya mipango.

Muheshimiwa katibu mkuu amekutana na muwakilishi wa Waziri wa mipango Dokta Maahir Hamadi Juhani na kujadili namna ya kushirikiana kati ya wizara na Ataba katika miradi ya sasa na baadae.

Muheshimiwa katibu mkuu amesikiliza maelezo kuhusu miradi tofauti inayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya kilimo, viwanda, mifugo na huduma zinazotolewa kwa mazuwaru watukufu.

Aidha ameambiwa miradi ya upanuzi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya, ili kuongeza ukubwa wa eneo la kutumiwa na mazuwaru hususan wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, kama mradi wa uwanja wa Ummul-Banina (a.s) utakaotumiwa na mazuwaru wa kike.

Wakazungumza pia kuhusu nafasi ya miradi ya Atabatu Abbasiyya ya kimkakati na viwanda, na jinsi inavyo saidia kutoa ajira kwa vijana wa Iraq sambamba na kukuza uchumi wa taifa.

Mheshimiwa Juhani akapata fursa ya kufanya ibada ya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: