Kitengo cha malezi na elimu ya juu kimetoa zawadi kwa washindi wa shindano la sikio Sikivu (Udhunul-Waaiyya).

Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimefanya hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la sikio sikivu.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na wimbo wa taifa pamoja na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa), halafu ikasomwa surat Faat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha yakafuata maigizo na qaswida za kidini zilizosomwa na wanafunzi.

Hafla ikahitimishwa kwa kugawa zawadi kwa wanafunzi wa kike na wakiume, waliopata nafasi za kwanza shuleni kwao na kwenye mashindano, kama sehemu ya kuwapongeza na kushajihisha wenzao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: