Nchini senegal.. Kitengo cha habari na utamaduni kimefanya mashindano ya Qur’ani.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya mashindano ya Qur’ani katika mji mkuu wa Senegal Dakaar, ikiwa ni sehemu ya program ya (Sufratul-Kafeel) inayofanywa barani Afrika.

Mashindano hayo yamesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo cha habari na utamaduni.

Muwakilishi wa Markazi nchini Senegal Shekhe Mustwafa Diba amesema “Tumefanya mashindano ya kwanza ya Qur’ani kwa wanafunzi wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s) pamoja na ndugu zetu wa madhehebu ya Sufi”.

Akaongeza kuwa “Idadi ya washiriki ilifika arubaini mbele ya kundi kubwa la wahudhuriaji kutoka vitongoji tofauti vya mji mkuu akiwemo mkuu wa mkoa wa Dakaar bibi Amina Manighi na maimamu wa misikiti sambamba na walimu wa Qur’ani”.

Akabainisha kuwa “Shindano lilibeba ujumbe wa amani baina ya waislamu pamoja na tofauti za madhehebu zao, na umuhimu wa kusaidiana katika wema na uchamungu kama inavyo sema Qur’ani ambayo ndio katiba ya waislamu wote”.

Rais wa Jumuiya ya Baitul-Izzah Shekhe Abdullatifu Jiin, ameshukuru Markazi kwa kuandaa mashindano haya kutokana na umuhimu wake wa kujenga mapenzi katika nafsi za raia wa Senegal.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: