Kituo cha utamaduni wa familia kinafanya ratiba ya mwezi wa Ramadhani kwa familia za mashahidi.

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kinafanya ratiba ya familia za mashahidi.

Mkuu wa kituo bibi Sara Hafaari amesema: “Ratiba imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa surat Faatiha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu”.

Akaongeza kuwa “Ratiba hiyo imehusisha utoaji wa muhadhara wenye anuani isemayo (Njia za kupata raha ya nafsi), mashindano ya kidini, majlisi ya kuomboleza, kusoma ziara ya Amini-Lahi na ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi familia zilizohudhuria”.

Kituo kinafanya juhudi kubwa katika ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani, kuhakikisha inajenga utamaduni wa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s), kwa mujibu wa maelezo ya Hafaari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: