Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kitongoji cha Karkha jijini Bagdad.
Hafla imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Bagdad chini ya Majmaa.
Hafla hiyo ni sehemu ya shughuli za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wasomaji mashuhuri wa Qur’ani tukufu wameshiriki kwenye hafla hiyo na imehudhuriwa na kundi kubwa la wapenzi wa Qur’ani.