Majmaa-Ilmi inaendelea na vikao vya usomaji wa Qur’ani kupitia ratiba ya Multaqa-Nurain.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na vikao vya usomaji wa Qur’ani kupitia ratiba ya Multaqa-Nurain.

Ratiba hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Baabil chini ya Majmaa kwa kushirikiana na uongozi wa mazaru ya Alawiyyatu-Sharifah (a.s).

Hualikwa wasomaji tofauti wa Qur’ani tukufu, vikao vya usomaji wa Qur’ani tukufu hufanywa ndani ya haram tukufu kwa muda wa mwezi mzima wa Ramadhani, vinahusisha mihadhara, nadwa, majlisi za kuomboleza na ibada za Lailatul-Qadri.

Aidha hufanywa mashindano mbalimbali yakiwemo mashindano ya Qur’ani, kuhifadhi hadithi arubaini kutoka kwa Ahlulbait (a.s), na kuhifadhi hekima arubaini za kiongozi wa waumini (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: