Mussawi atembelea shule za Al-Ameed.

Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na msimamizi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, ametembelea shule za Al-Ameed na kuangalia maendeleo yake.

Amepokewa na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Hassan Daakhil Hassanawi.

Mussawi ameangalia shughuli zinazofanywa na idara za shule katika sekta ya malezi na elimu, pamoja na mikakati ya baadae inayolenga uboreshaji wa sekta hiyo kama unavyo fanyika kimataifa.

Akasisitiza umuhimu wa kupatikana vifaa vyote vya lazima katika shule za Al-Ameed, na kuhakikisha tunaandaa kizazi kipya chenye uwezo wa kuleta maendeleo katika taifa letu pendwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: