Kitengo cha habari na utamaduni kinafanya hafla ya kuwapongeza walioshinda kwenye shindano la Qur’ani nchini Naijeria.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya hafla ya kugawa zawadi kwa washindi wa shindano la Qur’ani lililofanywa nchini Naijeria.

Shindano hilo liliandaliwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya na washindi waliteuliwa na jopo la majaji.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema kuwa tulifanya mashindano ya kuhifadhi Qur’ani nchini Naijeria siku za nyuma.

Akaongeza kuwa, leo tumefanya hafla ya kuwapongeza washindi na kuwapa zawadi mbele ya washiriki wenzao, wasomo wa Qur’ani na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Akasema: Program inaendelea katika bara la Afrika kwenye nchi tofauti na nyanja tofauti za kidini, Aqida, Fiqhi, Qur’ani, Akhlaq, ambapo husimamiwa na wawakilishi wa Markazi kwenye nchi zaidi ya ishirini na tano za Afrika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: