Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha mashindano ya vikundi awamu ya tano.
Mashindano hayo yalisimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Bagdad.
Jumla ya vikundi nane vimechuana kwenye mashindano hayo, ushindani ulikuwa katika usomaji, tajwidi, fiqhi na tafsiri mbele ya jopo la majaji.
Kikundi cha (Imamaini Askariyaini -a.s-) kimepata nafasi ya kwanza.
Mwisho wa mashindano hayo washiriki wamepewa zawadi na vyeti vya ushiriki, kama sehemu ya kuwahimiza waendelee kushiriki kwenye mashindano yajayo.