Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amekutana na viongozi wa Baabu-Khaan katika mji wa Karbala.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aaludhiyaau-Dini, amekutana na viongozi wa Baabul-Khaan katika mkoa wa Karbala.

Mkutano huo umehudhuriwa na kiongozi wa ofisi ya katibu mkuu, rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Muhammad Ali Azhar na baadhi ya viongozi wa Ataba tukufu.

Mheshimiwa katibu mkuu amesema, Hakika kukutana na viongozi wa Karbala kuna umuhimu mkubwa, kwani tunapata nafasi ya kubadilishana mawazo katika mambo yanayohusu mji wa Karbala.

Akaongeza kuwa “Katika mkutano tuliofanya na viongozi wa Baabu-Khani tumejadili mambo yanayohusu umuhimu wa mahusiano ya kijamii na namna ya kutumikia jamii katika nyanja tofauti”.

Akaendelea kusema kuwa, “Tumejadili nafasi ya Atabatu Abbasiyya katika kusaidia jamii ya watu wa Karbala, wahudhuriaji wakapongeza huduma zinazotolewa na Ataba katika jamii na mazuwaru wa mji huu mtukufu”.

Atabatu Abbasiyya tukufu inathamini sana vikao kama hivi, kwani vinasaidia kudumisha mawasiliano na watu wa Karbala na kutoa fursa ya kujadili mambo tofauti yanayohusu jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: