Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimehitimisha ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani iliyokuwa inahusu wanawake wa mji mtukufu wa Karbala.
Mkuu wa kituo bibi Sara Hafaar amesema, Ratiba ya mwezi wa Ramadhani ilihusu (chama cha usimamizi wa watoto) na (Rabitwa ya Ilimu Nuur) katika mkoa wa Karbala.
Akaongeza kuwa “Vikao vilikuwa vinafunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha inasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kurehemu mashahidi wetu, halafu unafuata mhadhara wenye anuani isemayo (Mbinu za kutengeneza furaha ya kweli) kutoka kwa Adhraa Ahmadi, kisha kulikuwa na majadiliano yaliyo ongozwa na bibi Ikhlasi Jawaad”.
Akahitimisha kwa kusema kuwa kituo kinaendelea kutoa huduma kwa makundi tofauti ya wanawake, kwa lengo la kuboresha familia za waislamu na kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).