Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimehitimisha ratiba ya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani katika mkoa wa Basra.
Ratiba hiyo imesimamiwa na kituo cha turathi cha mkoa wa Basra chini ya kitengo cha maarifa.
Ratiba hiyo ilianza kutekelezwa mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kusoma juzu moja kila siku katika kitongoji cha Baradhiiyya mkoani Basra.