Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ametoa zawadi kwa waadhini wa Ataba mbili tukufu.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aaludhiyaau-Dini, ametoa zawadi kwa waadhini wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Kikao cha utowaji wa zawadi kimehudhuriwa na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, ambao ni Sayyid Liith Mussawi, Sayyid Jawadi Hasanawi, Sayyid Mhandisi Muhammad Ashqar, kiongozi wa ofisi ya katibu mkuu, rais wa kitengo cha mahusiano Muhammad Ali Azhar.

Mheshimiwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Aaludhiyaau-Dini, amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na waadhini wa Ataba mbili tukufu wakati wote wa mwezi wa Ramadhani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: