Kitengo cha Maqaam kimetangaza kufanikiwa kwa ratiba yake maalum ya mwezi wa Ramadhani.

Kitengo cha Maqaam katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kufanikiwa kwa ratiba ya mwezi wa Ramadhani.

Msaidizi wa makamo rais Mhandisi Mahadi Muhammad Mussawi amesema “Kitengo kiliandaa ratiba maalum ya kuhudumia mazuwaru katika mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa “Ndani ya mwazi wa Ramadhani huwa tunaandaa ratiba maalum ya kuhudumia mazuwaru, kuanzia namna ya kusimamia uingiaji na utokaji ndani ya haram sambamba na kugawa futari na huwa tunaendelea kugawa chakula hadi katikati ya usiku, aidha huandaliwa sehemu maalum za kukaa mazuwaru”.

Maqaamu tukufu ya Imamu wa zama (a.f), imeshuhudia vikao vya usomaji wa Qur’ani, sambamba na kufungua vituo vya kutoa majibu ya kisheria, na kuandaa ratiba maalum ya kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) ndani ya mwezi wa Ramadhani, kama vile kuzaliwa kwa Imamu Hassan, kuuwawa kwa baba yake kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalid (a.s) na kuhuisha siku za Lailatul-Qadri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: