Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu pamoja na marais wa vitengo pia wameshiriki kupokea wageni waliokuja kutoa pongezi za sikukuu ya Idul-Fitri.
Mashekhe na viongozi mbalimbali wamemiminika katika Ataba tukufu kutoa pongezi za sikukuu hiyo.
Sambamba na pongezi hizo kwa wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wamemuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atupe amani na usalama katika taifa letu kipenzi.