Sayyid Swafi amempokea Shekhe Karbalai na wamepeana pongezi za Iddul-Fitri.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi leo siku ya Jumamosi asubuhi, amempokea kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekhe Abdulmahadi Karbalai na kupeana pongezi za Iddul-Fitri.

Mheshimiwa Shekhe Karbalai amekuja Atabatu Abbasiyya akiongozana na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Hassan Rashidi Al-Abaaiji, na baadhi ya viongozi wa Ataba tukufu.

Ugeni huo umepokewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aali Dhiyaau-Dini, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.

Katika kikao hicho wamepeana pongezi za sikukuu ya Iddul-Fitri, wakamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu alitunuku taifa letu amani na usalama.

Ataba imepokea mashekhe na viongozi wengi wa mkoa wa Karbala waliokuja kutoa pongezi za sikukuu hii tukufu, bila kusahau viongozi wa idara za ulinzi na usalama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: