Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amewapongeza wahudumu wa Atabatu Husseiniyya tukufu.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya na ujumbe wake, ametembelea uongozi mkuu wa Atabatu Husseiniyya na kutoa pongezi za sikukuu ya Idul-Fitri.

Mshauri wa katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Fadhili Auzi amesema kuwa Atabatu Husseiniyya na Ataba zingine zimejipanga vizuri katika siku za sikukuu, zinapokea wageni wanaokuja kufanya ziara maalum kwa bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuna ibada nyingi zinazofanywa katika siku kama hizi”.

Akaongeza kuwa: “Ugeni kutoka Atabatu Husseiniyya ulienda Atabatu Abbasiyya leo asubuhi na kupokewa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na maneno mazuri yakazungumzwa mbele ya wahudumu wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhul Abbasi (a.s)”.

Akafafanua kuwa “Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umetembelea malalo ya Imamu Hussein (a.s) na kupokewa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Dokta Alaa Ahmadi Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, wakapeana pongezi za sikukuu na kuahidi kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: