Kituo cha utamaduni wa familia kimetangaza kufanya semina.

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimetangaza kufanya semina ya wasichana inayo husu kujenga heshima.

Semina itakuwa na maudhui nyingi, miongoni mwa maudhui zake ni: Kutambua uhalisia, namna ya kujiepusha na hasira, mbinu za kushinda changamoto za maisha na namna ya kuhisi furaha katika maisha.

Semina itadumu kwa muda wa wiki mbili na wanafunzi wanatakiwa kuhudhuria darasani siku mbili kwa wiki, kuanzia saa tatu asubuhi hasi saa sita Adhuhuri, washiriki ni wasichana wenye umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

Kutakuwa na mtihani mwishoni mwa semina, watakao fanya vizuri watapewa zawadi, tambua kuwa washiriki ni idadi maalum pia kutakuwa na usafiri wa kuwachukua na kuwarudisha majumbani kwao.

Itatangazwa siku ya kuanza masomo baada ya kutimia idadi ya washiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: