Kitengo cha habari na utamaduni kimehitimisha ratiba ya kitamaduni katika mji wa Dhiqaar kwa wanufaika zaidi ya 100.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimehitimisha ratiba ya kitamaduni katika mji wa Dhiqaar.

Ratiba hiyo imesimamiwa na kituo cha Multaqal-Qamaru/ tawi la Dhiqaar chini ya kitengo.

Mkuu wa kituo Shekhe Harithi Dahi amesema “Ratiba ya kitamaduni iliyofanywa katika mji wa Dhiqaar, ilikuwa ni sehemu ya nadwa na mihadhara ya kitamaduni, inayotolewa na kitengo kwenye miji tofauti na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 100”.

Akaongeza kuwa “Ratiba ilikuwa na mihadhara miwili, wa kwanza uliarifu harakati za kituo na kutaja malengo na mikakati ya baadae, muhadhara wa pili ulihusu umuhimu wa turathi za kitamaduni na athari yake katika maendeleo ya watu”, akabainisha kuwa “Ratiba imehudhuriwa na viongozi wa kidini na kijamii”.

Akasema: “Shughuli iliyofanywa katika mji wa Nasri, inalenga kuelimisha jamii mambo yanayohusu utamaduni na Dini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: