Kijana huyo Sayyid Ghaith Ahmadi Maamuri amesema “Natanguliza shukrani za dhati kwa kiongozi mkuu wa kisheria, katibu mkuu Sayyid Mustwafa Aalu Dhiyaau-Dini, mjumbe wa kamati kuu Sayyid Jawaad Hasanawi kwa kukubali ombi langu na kunialika Ataba tukufu, baada ya mimi kutoa ombi kupitia moja ya televisheni”.
Akasema kuwa “Maombi yangu yamekubaliwa na uongozi wa Ataba tukufu ndani ya siku tano”.
Akaendelea kusema “Natoa shukrani za dhati kwa uongozi wa Atabatu Abbasiyya kwa msaada huu, hakika nashindwa kueleza furaha niliyonayo au kuwasilisha shukrani zangu katika jambo hili”.