Kila siku.. kitengo cha utumishi kinatandika mazulia katika maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya mazuwaru.

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kinatandika mazulia katika maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya kila siku kwa ajili ya mazuwaru, hususan siku za ziara maalum na siku za Ijumaa.

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Muhammad Harbi amesema “Kwa ajili ya kuandaa mazingira mazuri kwa mazuwaru, hususan katika siku za ziara maalum na siku za Ijumaa, wahudumu wa kitengo chetu hutandika mamia ya mazulia katika maeneo ya Jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambayo hushuhudia idadi kubwa ya mazuwaru”.

Akaongeza kuwa “Kazi ya kutandika mazulia inahusisha sehemu zilizo andaliwa na Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru, kwa kukaa na kupumzika Jirani na malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akabainisha kuwa “Kazi ya kuhudumia mazuwaru inafanywa chini ya utaratibu maalum ulioandaliwa na kitengo, ikiwa ni pamoja na kuandaa sehemu za kupumzika na kufanya ibada kwa amani na utulivu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: