Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimechapisha vitabu viwili, cha (Fiqhi ya mwanamke) na (Ibada ya Hija na viambatanishi vyake) kwa lugha ya Kiurdu.
Wasimamizi wa uchapishaji wa vitabu hivyo ni Maahadi ya turathi za Mitume tawi la Kiurdu chini ya kitengo.
Mkuu wa Maahadi Shekhe Husseini Turabi amesema “Wanafunzi kutoka Pakistani, wametafsiri vitabu viwili (Fiqhi ya mwanamke) na (Ibada ya Hija na viambatanishi vyake) kwa lugha ya Kiurdu ili kukidhi haja ya Kifiqhi katika sekta hiyo”.
Akaongeza kuwa “Vitabu vilivyo tafsiriwa vimeandikwa kwa mujibu wa fatwa za Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani na vinakubalika katika ofisi yake”.