Majmaa-Ilmi imetangaza ufunguzi wa semina ya kitaalamu kuhusu uandishi wa msahafu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kupitia Maahadi ya Qur’ani tawi la Najafu, imetangaza ufunguzi wa semina ya kitaalamu yenye anuani isemayo (Masomo kuhusu uandishi wa msahafu).

Washiriki watafundishwa historia ya msahafu, kanuni za uandishi, mitazamo yake na nakala zilizopo, mhadhiri wa semina hiyo ni Dokta Karim Zubaidi, washiriki wote wanatakiwa kuhudhuria moja kwa moja na nimaalum kwa wanaume tu.

Semina itaanza Jumatano ya tarehe kumi mwezi wa tano saa tisa jioni, itafanyika siku mbili kwa wiki, Jumapili na Jumatano kwa muda wa miezi miwili katika ofisi za Maahadi zilizopo (Najafu – mtaa wa Hanaanah – barabara ya Posta – Jirani na Husseiniyya ya Najjaar).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: