Idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya, inafanya mashindano ya (Mimbari za nuru) ya kuhifadhi Qur’ani.
Shindano holo linasimamiwa na shule ya Fatuma binti Asadi (a.s).
Washiriki ni wale waliohifadhi juzuu tatu, tano na kumi.
Shindano litafanywa mwezi wa sita tarehe (4 – 6) katika eneo la shule mtaa wa Mulhaq/ barabara ya hospitali ya Husseini/ kituo cha Swidiqah-Twahirah (a.s).
Atabatu Abbasiyya imeandaa zawadi kwa washindi wa tatu wa kila kundi, tambua kuwa washiriki ni wasichana tu.
Kwa maelezo zaidi piga simu namba (07602338401).