Idara ya wahadhiri imetangaza tarehe ya mashindano ya kuhifadhi Dua ya (Makarimul-Akhlaaq).

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imetangaza tarehe ya kufanya mashindano ya kuhifadhi dua ya (Makaarimul-Akhlaaq).

Mashindano yatafanywa siku ya Jumatano sawa na mwezi (26 Shawwal 1444h), kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba Adhuhuri.

Idara imeandaa zawadi nzuri kwa washindi watatu wa mwanzo, pia kutakuwa na zawadi kwa watu kumi wa mwanzo, iwapo watagongana basi mshindi atapatikana kwa njia ya kura.

Mashindano hayo yatafanywa katika ofisi za idara zilizopo Karbala -Mtaa wa Mulhaq- Jirani na chuo kikuu cha Swahibu-Zamaan (a.f), kituo cha Swidiqah-Twahirah (a.s), muda wa ushiriki unaanzia mwezi (21 Ramadhani) hadi (21 Shawwal).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: