Kitengo cha uboreshaji kimemaliza jaribio la semina ya kuhifadhi Nahajul-Balagha.

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kimemaliza jaribio la semina ya kuhifadhi Nahajul-Balagha kwa watumishi wa Ataba tukufu.

Rais wa kitengo Dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema: “Tumefanya jaribio la mwisho la semina ya kuhifadhi Nahajul-Balagha na sherehe yake, limedumu kwa miezi kadhaa, kwa muda wa saa mbili kila wiki”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kilichagua watu wanaopenda kushiriki katika watumishi wa Ataba, halafu wanapewa mihadhara kuhusu kuhifadhi Nahajul-Balagha na sherehe yake, kisha wakapewa vipande vya kuhifadhi”.

Akabainisha kuwa “Ratiba imekamilika kwa kuwapa jaribio na kubaini washindi miongoni mwao watakao shiriki kwenye shindano litakalo fanywa siku zijazo hapa Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: