Toleo jipya kutoka kitengo cha habari na utamaduni.. kitabu cha Almaad katika Qur’ani tukufu.

Hivi karibuni kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu cha (Almaad katika Qur’ani).

Uchapishaji wa kitabu hicho umesimamiwa na kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya kitengo.

Kitabu hicho kimeandika kuhusu masomo ya Aqida, juzu la kwanza limetafsiriwa na Dokta Ali Haji Hassan na juzu la pili limetafsiriwa na Dokta Muhammad Tarmas.

Kitabu kimeandikwa na Shekhe Abdullahi Aljawadi Al-Aamili, kinaeleza maswala ya kiyama na mambo yanayo fungamana na kiyama kwa kutumia nakili na akili.

Mada ya kiyama (Almaad) ni miongoni mwa mada muhimu sana katika somo la Aqida na falsafa, ameandika kwa undani kuhusu uwepo wake na mambo yanayofungamana na siku hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: