Ugeni wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, umehudhuria kwenye kongamano la balozi awamu ya kumi na mbili.
Ugeni huo umetoka Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu chini ya Majmaa.
Kongamano limefanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Kufa kielelezo cha Answari na kinara wa waarabu), katika kumbukumbu ya kuwasili Muslim bun Aqiil katika mji wa Kufa, mjumbe wa Imamu Hussein (a.s), chini ya ushiriki wa watafiti na washairi kutoka ndani na nje ya Iraq.
Kongamano limefanywa katika mkoa wa Najafu, limehudhuriwa na idadi kubwa ya viongozi wa Dini na wawakilishi wa taasisi mbalimbali.