Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kumbukizi ya uvunjwaji wa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya majlisi ya kumbukizi ya uvunjwaji wa makaburi ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) huko Baqii.

Majlisi imehudhuriwa na wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ilijaa huzuni kutokana na tukio hilo linalo umiza nyoyo za waumini.

Mhadhiri wa majlisi hiyo Sayyid Hassan Ghurabi amesema “Malalo ya Maimamu wa Baqii (a.s) yalivunjwa mara mbili: mara ya kwanza mwaka 1220 na mara nya pili 1344 hijiriyya, tukio hilo linahuzunisha waumini wote kutokana na ukubwa wa jinai zilizofanywa na wakufurishaji”.

Akasisitiza kuwa “Malalo hizo lazima zijengwe kwa sababu ni sehemu takatifu zilizobeba miili ya Maimamu waliotakaswa na Mwenyezi Mungu mtukufu, ukizingatia kuwa ni haram kuvunja heshima ya makaburi ya waislamu, kwani ni eneo takatifu ambalo hushuka Malaika wakati wote”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Ghurabi, Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi kadhaa za kuomboleza kutwa nzuma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: