Majmaa-Ilmi imeanza utekelezaji wa program ya (Arshu-Tilaawah).

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeanza kutekeleza program ya (Arshu-Tilaawah) ambayo hufanywa kila wiki ndani ya ukumbi wa haram ya Abbasi.

Program hiyo husimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.

Rais wa Majmaa Dokta Mushtaqu Ali amesema “Program inalenga kuibua na kulea vipaji vya usomaji wa Qur’ani ndani na nje ya Iraq sambamba na kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani”.

Akaongeza kuwa “Program ya leo imehudhuriwa na wasomi wa Qur’ani kutoka Iran pamoja na msomaji wa Atabatu Kadhimiyya Dokta Raafii Al-Aamiriy, ambapo ilikuwa ni ufunguzi wa program baada ya kusimama katika mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Kumbuka kuwa program inalenga kuibua vipaji kwa usomaji wa Qur’ani na kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii, kwa mujibu wa maelezo ya Dokta Ali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: