Watumishi wa Ataba mbili wanaomboleza kumbukizi ya kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s).

Watumishi wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kumbukumbu ya kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s) kwa kufanya matembezi ya pamoja.

Matembezi hayo yameanzia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba qaswida na mashairi ya kuomboleza, yanayo eleza tukio baya linaloumiza nyoyo za waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Baada ya matembezi hayo kuwasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s), wakafanya majlisi kubwa iliyo hudhuriwa na mazuwaru pia, zikasomwa qaswida na tenzi mbalimbali zilizotaja tukio hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: