Majmaa-Ilmi inatoa zawadi kwa washindi wa mradi wa kujenga uwezo.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inatoa zawadi kwa wanafunzi waliopata nafasi za kwanza kwenye mradi wa kujenga uwezo na walimu wao.

Hafla ya utowaji wa zawadi imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani na umefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Ali Osama, ikafuatiwa na ugawaji wa zawadi kwa washindi watatu waliopata nafasi za kwanza, mshindi wa kuhifadhi juzu tano, juzu kumi na juzu ishirini za Qur’ani tukufu.

Zawadi zimetolewa kwa wanafunzi na walimu, kwa lengo la kuwahamisha kuendelea na mradi huo mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: