Kitengo cha maarifa kinajadili na wageni kutoka kituo cha Alamah Hilliy njia za kuhuisha athari.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya pamoja na wageni kutoka kituo cha Alamah Hilliy chini ya Atabatu Husseiniyya wamejadili njia za kuhuisha athari.

Baada ya kupokewa ugeni huo wamejadili kwa pamoja namna ya kuhuisha turathi za wanachuoni wa Hillah, na njia za kuhuisha athari zao, aidha wameongea kuhusu kushirikiana na kushauriana katika kufanyia kazi malikale.

Mkuu wa kituo cha turathi za Hillah ameshukuru nakupongeza kazi nzuri inayofanywa ya uhakiki na uandishi, akawaomba waendelee na kazi hiyo tukufu yenye mchango mkubwa katika sekta ya elimu.

Wageni wamepongeza miradi ya uandishi wa vitabu na machapisho mbalimbali, inayofanywa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: