Balozi wa Brazili nchini Iraq amepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya.

Balozi wa Brazili nchini Iraq Mheshimiwa Luwis Santos, amepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya kataika sekta ya afya, viwanda, elimu, na huduma za kibinaadamu zinazotolewa kwa mazuwaru.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Balozi wa Brazili ametembelea baadhi ya miradi ya Ataba akiwa na rais wa kitengo cha uhusiano na mkuu wa ofisi ya katibu mkuu, wameangalia miradi ya afya, elimu, viwanda na vituo vingine vilivyo chini ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Ziara hiyo imehusisha kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambapo Mheshimiwa Balozi amevutiwa na mazingira mazuri ya kiroho yaliyopo, akapongeza mpangilio na utendaji wa shughuli za Ataba”.

Mheshimiwa Santos amesema “Nimetembelea mji mtukufu wa Karbala, nimevutiwa na maendeleo makubwa ya viwanda na shughuli zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya, ambazo zinachangia uchumi wa taifa na kupunguza uhaba wa chakula, miradi hii inaonyesha maono makubwa ya kuendeleza taifa la Iraq na raia wake katika sekta tofauti”.

Akaongeza kuwa: “Ninafuraha kubwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya, nimatumaini yangu ushirikiano huu utaendelea kuimarika zaidi kupitia mikataba tunayoendelea kusaini” akasema “Kufikiria vyanzo tofauti vya mapato ni jambo zuri sana, kikiwemo chanzo cha kilimo na viwanda”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: