Maukibu ya watu wa Karbala imehuisha kumbukumbu ya kubomolewa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s) kwa kufanya matembezi ya pamoja kwa mara ya kwanza katika tukio hili.
Matembezi hayo yamefanywa kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, aidha wahudumu wa Ataba hizo pia wameshiriki pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama wakiwemo wapiganaji wa kikosi cha Abbasi, Ali Akbaru na walinzi wa haramaini tukufu.
Matembezi yameanzia barabara ya Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), bendera za Maimamu wa Baqii zikapandishwa mbele ya mlango wa Qibla, kisha msafara ukapitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba Qaswida za kuomboleza zinazoeleza tukio hilo baya linaloumiza nyoyo za wapenzi wa Ahlubait (a.s).
Baada ya kuwasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) wakafanya majlisi ya kuomboleza iliyopambwa na Qaswida kutoka kwa Ali Waailiy, Qaswida nyingi zimehimiza ujenzi wa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s), na tenzi za Husseiniyya zikaeleza tukio hilo baya.