Sayyid Swafi amehusia kuongeza juhudi za kufanikisha mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amehusia kuongeza juhudi za kufanikisha mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu na Maahadi za Iraq kwa mwaka wa masomo 2023.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mahafali Sayyid Maahir Khalidi amesema “Kamati imemuambia Mheshimiwa Sayyid Swafi, katibu mkuu wa Ataba tukufu Sayyid Mustafa Aalu Dhiyaau-Dini, wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo kuhusu maandalizi yanayoendelea, na ikasikiliza maelekezo ya Mheshimiwa kuhusu mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu na umuhimu wa jambo hilo”.

Akaongeza kuwa “Maandalizi ya mahafali yanahusisha kuandaa sehemu za malazi ya wanafunzi, kutengeneza vitambulisho maalum, zawadi na ujumbe mkuu utakaotolewa wakati wa mahafali”, akabainisha kuwa “Mahafali ya awamu ya pili yatakuwa na kauli mbiu isemayo (Kutoka ardhi ya Karbala ukarimu umechanua), kundi la (Juu ya uongofu wa mwezi awamu ya pili), nayo ni sehemu ya harakati za mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, shughuli hii inatokana na kitengo cha mahusiano”.

Khalidi akasema kuwa “Katika mahafali haya vitashiriki zaidi ya vyuo (34) kutoka mikoa ya kaskazini, kusini na kati, mahafali itaonyesha picha halisi ya mwanafunzi wa chuo kikuu na namna anavyo ingia katika Maisha ya kijamii baada ya kuhitimu chuo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: