Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya kimefanya maboresho ya nne katika toghuti ya Baqii-Gharqad, kufuatia kumbukizi ya uvunjwaji wa makaburi ya Maimamu wa Baqii.
Kiongozi wa idara ya program Sayyid Haidari Abdu-Auni amesema “Tangu kuanzishwa kwa toghuti hii miaka 12 iliyopita, imeshafanyiwa maboresho mara kadhaa na kuifanya iendane na maendeleo yaliyopo, hivi sasa tumeifanyia maboresho kwa mara ya nne sambamba na kumbukizi ya uvunjwaji wa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Maboresha ya sasa yanatofautiana na maboresho yaliyopita, hakika yanaendana na maendeleo ya toghuti ya kipindi hiki”.
Kwa mujibu wa Abdu-Aun, maboresho yote yamefanywa na wataalamu wa idara ya wahandisi wa mitandao chini ya kitengo, bila kutegemea msaada wowote kutoka nje.