Kitengo hicho kinafanya kazi kwa kushirikiana na kitengo kama hicho cha Atabatu Husseiniyya tukufu, kwa pamoja wamejipanga kusimamia matembezi ya wanafunzi watakaoshiriki kwenye mahafali hiyo, watakapoenda kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na shughuli zingine za mahafali zitakazo fanyika.
Aidha kitengo cha kulinda nidham kitaratibu matembezi ya kuingia ndani ya Atabatu Abbasiyya na shughuli zitakazo fanywa katika shule za Al-Ameed sambamba na kuhakikisha usalama wa wanafunzi hadi watakaporudi kwao.
Vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya vinavyo husika na shughuli hiyo, vinafanya maandalizi makubwa ya kufanikisha mahafali hiyo ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.