Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinaendelea kujiandaa kwa ajili ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu.

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya halam mbili katika Atabatu Abbasiyya, kinaendelea na maandalizi ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu awamu ya pili.

Kitengo kinamkakati maalum wa utekelezwaji wa mahafali hiyo, kitaongoza matembezi ya wahitimu wakati wa kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s) kwa kupitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na wakati wa kwenda kwa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Matembezi yataongozwa na timu ya watumishi sambamba na kuweka vizuwizi kwa ajili ya kuzuwia kuingiliana na mazuwaru wakati wa mahafali.

Vitengo vya Atabatu Abbasiyya vinavyo husima na mahafali hiyo vipo katika maandalizi makubwa ya kuhakikisha mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu inafanikiwa kwa ufanisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: