Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amehimiza kukamilisha maandalizi.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, amehimiza kukamilisha maandalizi ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq mwaka 2023.

Ameyasema hayo kwenye kikao alichofanya na kamati ya maandalizi, inayojumuisha wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya, marais wa vitengo vinavyo husika na mahafali hiyo na manaibu wao.

Sayyid Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Watu wengi wanafatilia shughuli za Atabatu Abbasiyya, hivyo lazima tujitahidi kufanya mambo kwa ufanisi na tuhakikishe mahafali ya wahitimu inafana” akabainisha kuwa “Kazi iliyofanywa siku za nyuma na inayoendelea kufanywa na wajumbe wa kamati kuu inalenga kufanikisha mahafali haya kwa ufanisi mkubwa”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya ni shule, imefanikiwa kutoa wahitimu wengi kwenye sekta tofauti” akasisitiza kuwa “Katika matukio kama haya tunatakiwa kunufaika nayo katika sekta zote, habari, utumishi, uhandisi nk”.

Akaendelea kusema “Tunatakiwa kuandika kila changamoto itakayojitokeza wakati wa utekelezaji kwa ajili ya kutafuta utatuzi wake, mafanikio hutokana na kufanya kazi kwa juhudi na umoja, hakika mahafali hii itaacha athari katika nyoyo za wanafunzi na itakuwa msingi wa kujenga taifa hili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: