Kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa idadi kubwa ya basi zake kwa ajili ya kubeba washiriki wa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq, kuwachukua na kuwarudisha majumbani mwao.
Basi hizo zinawachukua washiriki kutoka mikoa tofauti na kuwapeleka Karbala.
Gari za wanafunzi zitawachukua wageni na kuwapeleka sehemu ya kupumzika katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya uliopo barabara ya (Karbala – Najafu) na kwenye jengo la Shekhe Kuleini lililopo barabara ya Bagdad katika mkoa wa Karbala.
Vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu vinafanya maandalizi makubwa ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.