Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imetoa zawadi kwa walimu na wasomaji walioshiriki kwenye harakati zake za mwezi wa Ramadhani katika mji mkuu wa Bagdad.
Zawadi zimetolewa katika hafla ya usomaji wa Qur’ani iliyofanywa na tawi la Bagdad chini ya Majmaa wilaya ya Husseiniyya kaskazini mashariki ya Bagdad.
Utoaji wa zawadi kwa walimu na wasomi walioshiriki kwenye ratiba ya mwezi wa Ramadhani ni sehemu ya kuonyesha thamani ya kazi kubwa waliyofanya katika mwezi huo mtukufu, kazi ya kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani tukufu katika jamii za watu tofauti.
Maahadi inaendelea kuandaa mashindano, nadwa, vikao vya usomaji wa Qur’ani katika kipindi chote cha mwaka, kwa lengo la kueneza utamaduni wa kushikamana na vizito viwili katika jamii.