Rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu amesema: Ataba tukufu inafanya mahafali ya mfano ya wahitimu wa vyuo vikuu.

Rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi amesema kuwa, Ataba tukufu inafanya mahafali ya mfano kwa wahitimu wa vyuo vikuu.

Ameyasema hayo pembezoni mwa kikao cha kamati ya maandalizi kilicho hudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, akaongeza kuwa: kikao cha leo ni miongoni mwa vikao vya mwisho mwisho katika maandalizi ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu, ifahamike kuwa wahitimu elfu moja kutoka vyuo tofauti watashiriki kwenye mahafali hiyo.

Mahafali inalenga kuleta mabadiliko katika ulimwengu wa vijana na kuwajenga kimaadili.

Akafafanuwa kuwa, vyuo vikuu vya Iraq vimeanza kuiga tabia za kimagharibi na kuacha misingi ya tamaduni za kiislamu, kwa mujibu wa ripoti zinazoandikwa na mitandao ya kijamii, hivyo Ataba tukufu inalenga kufanya kampeni ya kurudisha misingi za kiislamu kupitia mahafali hii.

Kwa mujibu wa Mussawi, Atabatu Abbasiyya inafanya mahafali ya mfano kwa wahitimu na familia zao, kwani wahitimu wapo katika kipindi cha mabadiliko ya kutoka kwenye Maisha ya chuo na Kwenda kufanyia kazi elimu waliyopata.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: