Kwa picha.. kuwasili kwa misafara ya washiriki wa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.

Kuwasiri wa misafara ya washiriki wa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq awamu ya pili, inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya kesho siku ya Ijumaa.

Kituo cha kwanza ni katika jengo la Atabatu Abbasiyya lililopo barabara ya Najafu, baada ya kukamilika kwa maandalizi ya kuwapokea.

Kitengo cha utalii wa kidini katika Ataba tukufu kimeshiriki kuwatoa majumbani kwao na kuwaleta Karbala kwa ajili ya mahafali itakayo fanyika kesho siku ya Ijumaa jioni.

Gari hizo zitatumika kuwapeleka sehemu zote watakazo pangiwa kutembelea na baada ya ratiba kukamilika zitawarudisha majumbani kwao.

Vitengo vinavyo husika na mahafali hii, vimejiandaa vizuri na vitahakikisha mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu inafana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: