Kukamilika kwa ushonaji wa mamia ya vitambaa na bendera zitakazotumika kwenye mahafali ya wahitimu wa chuo kikuu.

Kitengo cha kupokea zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha ushonaji wa mamia ya vitambaa na bendera zitakazo tumika kwenye mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.

Kiongozi wa idara ya ushonaji Sayyid Abduzahara Daudi Salmaan amesema “Watumishi wa idara yetu wameshona zaidi ya vitambaa elfu moja vitakavyo tumika kwenye mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq”.

Akaongeza kuwa “Vitambaa hivyo vimeshonwa kwa mashine za kisasa na kuwekwa mapambo na maandishi”.

Vitambaa vilivyo tumika vinaubora mkubwa.

Vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya vinaendelea na maandalizi makubwa katika ngazi zote za mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: